Jumatano, 26 Machi 2014

ZIARA YA UBALOZI WA MAREKANI KATIKA HOSPITALI TEULE YA RUFAA YA MKOA WA PWANI (TUMBI) KIBAHA










MATUKIO KATIKA HAFLA FUPI YA MENEJIMENTI YA SHIRIKA KUMUAGA ALIYEKUA MKURUGENZI WA FEDHA NA UHASIBU NDUGU PETER SILAS MSANGI ALIYESTAAFU KWA MUJIBU WA SHERIA

 Wajumbe wa Menejimenti ya Shirika wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba, wakiwasili katika eneo maalumu lililoandaliwa kwa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mstaafu wa Fedha na Uhasibu Ndugu Peter Silas Msangi akiwasili chini ya mapokezi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Hafla hiyo Ndugu Alexander Kashaija.

 Akifungua 'Shampeni' iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake kumtakia afya njema katika maisha yake ya kustaafu.


 Muda wa Chakula.

 Mkono wa Kheri.

 
 Katika picha za pamoja.

 
 
 
 Muda wa kulisakata Rhumba kumtakia maisha mema baada ya kustaafu.

SAFARI YA MWISHO YA NDUGU WILSON HEZRON MASWAGA ALIYEKUWA MTUMISHI WA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA

 
Ndugu Wilson Hezron Maswaga
Enzi za Uhai Wake
 
 
Safari ya kumfikisha ndugu yetu Wilson Hezron Maswaga katika nyumba yake ya kudumu ilikumbwa na vikwazo kadhaa kutokana na uharibifu wa miundombinu kuelekea kijijini Mseta, Mpwapwa-Dododma.

Jeneza lenye mwili likiwa limehifadhiwa katika nyumbani kwao mara baada ya kuwasili.

Mke wa Marehemu Wilson Hezron Maswaga (Katikati) akiwa pamoja na mama wa marehemu (Kulia) na ndugu wa karibu (kushoto) kijijini Mseta wakati ibada ya kumuombea marehemu kabla ya mazishi ikiendelea.

Zoezi la heshima za mwisho na kumuaga marehemu likiendelea chini ya uangalizi wa karibu wa watumishi wa Shirika.

Ibada ya mazishi ikiendelea chini ya watumishi wa Kanisa la Anglikana.

Nyumba ya milele alimolazwa Ndugu Wilson Hezron Maswaga katika makaburi ya kijiji cha Mseta, Wilayani Mpwapwa-Mkoani Dodoma.

Jumatano, 19 Machi 2014

MTOTO DANIEL EMMANUEL LYMO ATELEKEZWA MBEZI MWISHO JIJINI DAR ES SALAAM NA YUPO TUMBI HOSPITALI KIBAHA PWANI KWA MATIBABU





Mtoto Daniel Emmanuel Lymo (12) yupo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani (Tumbi), akiuguza majeraha ya mkono alioumizwa kwa kipigo cha watu wasiojulikana Mbezi jijini Dar Es Salaam baada ya kutelekezwa na mama yake mdogo (Gladies) aliyesafiri nae wakitokea Marangu (Himo) baada ya kumwambia kuwa anampeleka kwa bibi yake jijini Dar kwa bus la Dar Express (kwa mujibu wa mtoto), Baba alishafariki siku nyingi, mamaye ana taarifa kuwa anaishi Morogoro ila hajawai muona tangu akiwa mdogo....Aidha, amedai mpaka tukio hili linamkuta alikua akisoma katika Shule ya Msingi ya Kiingereza Marangu Hills darasa la nne (4). Kwa yeyote mwenye kumfahamu tafadhali saidia kupata msaada wa kumsaidia kupata nduguze kupitia:
+255-779-957-140.
Aksanteni

Jumatano, 5 Machi 2014

MKUTUBI MKUU MPYA WA MAKTABA YA UMMA YA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA ATAMBULISHWA RASMI KWA MKURUGENZI MTENDAJI MKUU WA SHIRIKA

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ndg.Suzanne Cassian Kibozi (kulia) akimtambulisha kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (katikati), Mkutubi Mkuu Mpya wa Maktaba ya Umma ya Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Jackton B. Kaijage (kushoto) mapema leo asubuhi.

 
Mkutubi Mkuu Mpya wa Maktaba ya Umma ya Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Jackton B. Kaijage (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (anayeshuhudia pichani) mapema leo asubuhi.

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ndg.Suzanne Cassian Kibozi (kulia), Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (katikati), na Mkutubi Mkuu Mpya wa Maktaba ya Umma ya Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Jackton B. Kaijage (kushoto) mapema leo asubuhi wakijadili baadhi ya mambo wakati wa zoezi hilo la utambulisho.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (pili toka kulia), aliyekuwa Kaimu Mkutubi Mkuu wa Maktaba hiyo Ndg.Clavery Chausi (aliyekupa mgongo), Afisa Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani Shirikani Ndg.Ally Salehe Lumango (wa kwanza kulia), pamoja na Mkutubi Mkuu Mpya wa Maktaba ya Umma ya Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Jackton B. Kaijage (pili toka kushoto) mapema leo asubuhi wakiendelea na taratibu la utambulisho.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (kulia), akitoa maelekezo ya kiutendaji na ushirikiano katika kazi kwa aliyekuwa Kaimu Mkutubi Mkuu wa Maktaba hiyo Ndg.Clavery Chausi (kushoto), Afisa Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani Shirikani Ndg.Ally Salehe Lumango (aliyekupa mgongo), pamoja na Mkutubi Mkuu Mpya wa Maktaba ya Umma ya Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Jackton B. Kaijage (anayekutazama) mapema leo asubuhi wakati wa zoezi la utambulisho.

Aliyekuwa Kaimu Mkutubi Mkuu wa Maktaba ya Umma ya Shirika la Elimu Kibaha, Ndg.Clavery Chausi (kushoto), pamoja nae Mkutubi Mkuu Mpya wa Maktaba ya Umma ya Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Jackton B. Kaijage (kulia), wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (hayupo pichani), mapema leo asubuhi wakati wa zoezi la utambulisho.

Jumatatu, 3 Machi 2014

AFISA MKUU MPYA WA MILIKI SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA ATAMBULISHWA KWA MKURUGENZI MTENDAJI MKUU WA SHIRIKA


 Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ndg.Suzanne Cassian Kibozi (katikati) akimtambulisha kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (kushoto), Mkuu Mpya wa Miliki na Majengo wa Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Sephania Solomon Mwakabengele (kulia) mapema leo asubuhi.
 
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (kushoto), akipeana mkono wa salamu na ukaribisho Shirikani na Mkuu Mpya wa Miliki na Majengo wa Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Sephania Solomon Mwakabengele (aliyesimama) mapema leo asubuhi.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (kushoto), akizungumza kwa pamoja na aliyekua Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Miliki na Majengo Ndg.Zakaria Mwinuka (shati la rangi ya damu ya mzee), Mkuu Mpya wa Miliki na Majengo wa Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Sephania Solomon Mwakabengele (anayeandika), pamoja na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani Ndg.Salehe Ally Lumango (anayetazamana na aliyekua Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Miliki na Majengo) leo.

Wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba (hayupo pichani), aliyekua Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Miliki na Majengo Ndg.Zakaria Mwinuka (kushoto), na Mkuu Mpya wa Miliki na Majengo wa Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Sephania Solomon Mwakabengele (kulia).
 
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika Dk.Cyprian G. Mpemba, akiendelea na mazungumzo ya pamoja ya utambulisho kwa aliyekua Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Miliki na Majengo Ndg.Zakaria Mwinuka (shati la rangi ya damu ya mzee), Mkuu Mpya wa Miliki na Majengo wa Shirika la Elimu Kibaha Ndg.Sephania Solomon Mwakabengele (kwanza kushoto), pamoja na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani Ndg.Salehe Ally Lumango (pili kushoto) leo asubuhi.

MWANDISHI WA HABARI NA MTANGAZAJI WA KITUO CHA RUNINGA CHA CHANNEL TEN NDG.SALUM MKAMBALA AFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA PWANI (TUMBI) BAADA YA AJALI YA MAGARI KUGONGANA VIGWAZA-CHALINZE

Ndg.Salum Mkambala akipatiwa matibabu mara baada ya kuwasilishwa na wasamaria wema kutoka katika eneo la tukio, huku nduguye Idd Mkambala (mwenye fulana nyeupe na mstari mwekundu) akifuatilia huduma hiyo kwa karibu.

Wataalamu wa Afya (Madaktari na Wauguzi) wakiendelea kumpa matibabu ya awali ya haraka Ndg.Salum Mkambala mara baada ya kuwasilishwa na wasamaria wema kutoka katika eneo la tukio.